← Back to Updates

Kituo Cha Great Passion Orphanage Centre kipo Vikindu

BY ILARIO CATRECE THEODORY — FRI, 01-NOV-2024, 19:39
Kituo Cha Great Passion

Event Details

Kituo hiki kinaongozwa na Baba ambaye amejitolea kuwalea watoto hawa; hakina wafanyakazi wa kuwalea watoto hao isipokua Baba huyo. Wakati mwingine watoto hujiweza kuwalea wenyewe kwani wamelelewa vidhuri mno. Sifa kubwa ya watoto hawa ni hospitality — wanapokea wageni kwa upendo na hufurahia kila msaada.

HITAJI NO 1. CHAKULA — Chakula ni kitu muhimu sana; kuna uhaba mkubwa wa chakula chini ya stoka yao. HITAJI NO 2. VIFAA VYA SHULE — watoto wanahitaji vifaa na usafiri ili kufika shule. HITAJI NO 3. NGUO — nguo za ndani na nguo za shule zinahitajika. HITAJI NO 4. VITANDA NA MAGODORO — watoto walikuwa wakilala chini kabla ya kupata vitanda. HITAJI NO 5. HUDUMA YA AFYA — dawa na kiti cha kwanza (first aid kit) kwa dharura.

Tarehe ya tukio ilitajwa kuwa 28 December 2024 kama siku ya kufunga mwaka — shiriki pamoja kutimiza lengo letu.


Source: youthcharityfoundation.com.free